Monday, 12 June 2017

Hakika kwa hili la uwizi wa rasilimali za taifa, ni lazima kila mtanzania mwenye nia dhabiti na nchi yake   amuunge Mh Rais wetu mkono katka mapambano haya. Vita hii ni kubwa ni lazima wote tushikamne kupinga uporaji unaofanywa na wachache wa kutumia rasilimali zetu kwa manufaa yao wenyewe.
Mh Rais ninakupongeza sana kwa hatua unazochukua,hakika nia yako ya kulikomboa taifa imedhirika wazi, na ninakuombea kwa mwenyzi mungu azidi kukupa nguvu, uzima na afya ili uweze kutuleta maendeleo.

Thursday, 8 June 2017

UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Jinsi uharibifu wa mazingira unavyoenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.Uharibifu huu unasababishwa na shughuli za ukataji mikaa,upanuzi wa maeneo ya kilimo ya usiozingatia sera,sheria, kanuni na taratibu

Vitendo vya uchomaji moto,ukataji miti unavyoenea
 katika maeneo mengi wilayani Kibondo 2016
.

UFUGAJI WA ASILI

Ufugaji wa asili  ni ufugaji ambao hufanyika katika maeneo huru kwa kuzingatia utaalamwa wa asili.Aina ya ufugaji huu umekuwa ukiwasaida  jamii kubwa ya watanzania kitika kufanya shughuli za kimaisha shughuli hizo ni kama vile kugharamia huduma za matibabu,chakula na mavazi,kugharamia huduma za elimu na shughuli nyinginezo.

kundi la mbuzi na kondoo katika kijiji cha  Terat 
Wilayani Simanjiro Aprili 2014

PROGRAM YA UTENGAJI MAENEO YA MALISHO YA MIFUGO

Wataalam na wanachi wa vijjij vitatu Ngapapa,Lerug na Orkitikiti wakiwa katka mikutano ya kutenga maeneo ya malisho na kilimo.programu hii  infadhiliwa na shirika la SIDA kupitia wizara ya mifugo na kilimo. Mradi huu unajulikan kw jina la OLENGAPA

  
Wataalam wa mifugo wakiwasili katika mikutano ya uhamasishaji
katika vijiji vya  Lerug,Ngapapa na Orkitikiti


 
    Wataalam wa mifugo wakifafanua jinsi mchakato wa utengaji wa maeneo 
ya malisho, kilimo na misitu inavyotengwa kwa mujibu wa sera na sheria


Wanachi wakiwa katika mkutano  wa pamoja wakiwasikilaza kwa 
 makini wataalam toka katika halmashauri ya wilaya ya Kiteto na wizara ya
 mifugo.kampeni za uhamasishaji zilizofanyika mwezi Juni 2015


TAMBIKO LA JAMII YA KIMASAI

Kufanya matambiko  katika mila ya jamii ya kimasai ni muhimu sana kutokana na imani na
utaratibu wa kila koo. Shughuli hizi huwa zinafanywa kwa muda maalum na kila koo.
Mfano ukoo wa Molel Tambiko huwa linafanywa mwanzoni mwa mwaka kwa ajili
ya kuomba neema za ALLAH katika mwaka husika.Ukoo wa Laizer wao hufanya
katikati ya mwaka kuashiria kipindi cha mavuno,majani kukauka na kuomba fadhila
kwa Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho.
 Mzee Ndaadu Oloipuki akifanya tambiko katika sherehe za kumsika
 uzee Bw.Arangai Olekonor katika kijjij cha Orpopong'i wilayani kiteto June 2014.

UTAMADUNI WA KIMASAI


 Namna au jnsi ya kuandaa chakula katika utamaduni wa jamii ya kimasai.Jinsi ya kuandaa maziwa yamgando au mabichi ni tofauti na jinsi ya kuandaa  nyama choma.Nyama choma  katika jamii ya kimasai huwa inaandaliwa maalum ikiwepo kuandaa eneo la kuchomea,kuandaa kuni,na madawa ya asili ya kuwekwa nyama kabla ya kuchomwa.Uchomaji nyama hufanywa na kundi maalum la watu wenye utaalam wa jinsi ya kuchoma nyama kiasili.

.
Jinsi ya kuandaa chakula aina ya nyama choma katika jamii ya kimasasi tukio
 lilofanyika katika kijiji cha Terat  wilayani Simanjiro  August 2016

WANYAMA DUME BORA

Ufugaji bora hutegemea madume bora yenye mbegu ambayo yameendaliwa ili kuweza  kukabiliana na mazingira kame pamoja  na aina ya mifugo ambayo madume hayo yanaandaliwa. Madume bora husaidia wafugaji kuwa na mifugo bora ambayo hukua kwa muda mfupi.

Dume aina ya Boran ambayo amechukuliwa katika kambi ya mifugo ilyopo Tengeru 2013.

Hakika kwa hili la uwizi wa rasilimali za taifa, ni lazima kila mtanzania mwenye nia dhabiti na nchi yake   amuunge Mh Rais wetu mkono katka...