Hakika kwa hili la uwizi wa rasilimali za taifa, ni lazima kila mtanzania mwenye nia dhabiti na nchi yake amuunge Mh Rais wetu mkono katka mapambano haya. Vita hii ni kubwa ni lazima wote tushikamne kupinga uporaji unaofanywa na wachache wa kutumia rasilimali zetu kwa manufaa yao wenyewe.
Mh Rais ninakupongeza sana kwa hatua unazochukua,hakika nia yako ya kulikomboa taifa imedhirika wazi, na ninakuombea kwa mwenyzi mungu azidi kukupa nguvu, uzima na afya ili uweze kutuleta maendeleo.
KINYIKINYI
Monday, 12 June 2017
Thursday, 8 June 2017
UHARIBIFU WA MAZINGIRA
Vitendo vya uchomaji moto,ukataji miti unavyoenea
katika maeneo mengi wilayani Kibondo 2016
katika maeneo mengi wilayani Kibondo 2016
.
UFUGAJI WA ASILI
kundi la mbuzi na kondoo katika kijiji cha Terat
Wilayani Simanjiro Aprili 2014
PROGRAM YA UTENGAJI MAENEO YA MALISHO YA MIFUGO
Wataalam wa mifugo wakiwasili katika mikutano ya uhamasishaji
katika vijiji vya Lerug,Ngapapa na Orkitikiti
Wataalam wa mifugo wakifafanua jinsi mchakato wa utengaji wa maeneo
ya malisho, kilimo na misitu inavyotengwa kwa mujibu wa sera na sheria
Wanachi wakiwa katika mkutano wa pamoja wakiwasikilaza kwa
makini wataalam toka katika halmashauri ya wilaya ya Kiteto na wizara ya
mifugo.kampeni za uhamasishaji zilizofanyika mwezi Juni 2015
TAMBIKO LA JAMII YA KIMASAI
Kufanya matambiko katika mila ya jamii ya kimasai ni muhimu sana kutokana na imani na
utaratibu wa kila koo. Shughuli hizi huwa zinafanywa kwa muda maalum na kila koo.
Mfano ukoo wa Molel Tambiko huwa linafanywa mwanzoni mwa mwaka kwa ajili
ya kuomba neema za ALLAH katika mwaka husika.Ukoo wa Laizer wao hufanya
katikati ya mwaka kuashiria kipindi cha mavuno,majani kukauka na kuomba fadhila
kwa Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho.
utaratibu wa kila koo. Shughuli hizi huwa zinafanywa kwa muda maalum na kila koo.
Mfano ukoo wa Molel Tambiko huwa linafanywa mwanzoni mwa mwaka kwa ajili
ya kuomba neema za ALLAH katika mwaka husika.Ukoo wa Laizer wao hufanya
katikati ya mwaka kuashiria kipindi cha mavuno,majani kukauka na kuomba fadhila
kwa Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho.
Mzee Ndaadu Oloipuki akifanya tambiko katika sherehe za kumsika
uzee Bw.Arangai Olekonor katika kijjij cha Orpopong'i wilayani kiteto June 2014.
UTAMADUNI WA KIMASAI
Namna au jnsi ya kuandaa chakula katika utamaduni wa jamii ya kimasai.Jinsi ya kuandaa maziwa yamgando au mabichi ni tofauti na jinsi ya kuandaa nyama choma.Nyama choma katika jamii ya kimasai huwa inaandaliwa maalum ikiwepo kuandaa eneo la kuchomea,kuandaa kuni,na madawa ya asili ya kuwekwa nyama kabla ya kuchomwa.Uchomaji nyama hufanywa na kundi maalum la watu wenye utaalam wa jinsi ya kuchoma nyama kiasili.
.
Jinsi ya kuandaa chakula aina ya nyama choma katika jamii ya kimasasi tukio
lilofanyika katika kijiji cha Terat wilayani Simanjiro August 2016
WANYAMA DUME BORA
Ufugaji bora hutegemea madume bora yenye mbegu ambayo yameendaliwa ili kuweza kukabiliana na mazingira kame pamoja na aina ya mifugo ambayo madume hayo yanaandaliwa. Madume bora husaidia wafugaji kuwa na mifugo bora ambayo hukua kwa muda mfupi.
Dume aina ya Boran ambayo amechukuliwa katika kambi ya mifugo ilyopo Tengeru 2013.
Subscribe to:
Comments (Atom)
Hakika kwa hili la uwizi wa rasilimali za taifa, ni lazima kila mtanzania mwenye nia dhabiti na nchi yake amuunge Mh Rais wetu mkono katka...
-
Kufanya matambiko katika mila ya jamii ya kimasai ni muhimu sana kutokana na imani na utaratibu wa kila koo. Shughuli hizi huwa zinafany...
-
Ufugaji bora hutegemea madume bora yenye mbegu ambayo yameendaliwa ili kuweza kukabiliana na mazingira kame pamoja na aina ya mifugo ambay...
-
Namna au jnsi ya kuandaa chakula katika utamaduni wa jamii ya kimasai.Jinsi ya kuandaa maziwa ya mgando au mabichi ni tofauti na jinsi ya ...
